Tuesday 18 March 2014

LEO NYASI BILA SHAKA ZITAUMIA.



                Tue 18/03/2014
                UEFA CL Round of 16 (2nd leg)
Ama kweli leo kiama katika ligi ya mabingwa ulaya. Ni Drogba uso kwa uso na the special one. Ikumbukwe kwamba Chelsea maarufu kama the blue, wameweza kuchakua ubingwa wa CL kwa juhudi binafsi za Didier ambaye kumbukumbu zangu zaniambia alisawazisha kwa kichwa goli lililopigwa mithili ya mashuti ya aliyekuwa beki ngangari na kisiki wa Brasil- the Roberto Carlos.Goli hilo liliwapeleka katika penati ambapo Drogba alipiga penati ya mwisho iliyojaa kimyani na kuandika ubingwa kwa mara ya kwanza katika CL.
Hii leo bila shaka mechi itakuwa ya kuvutia kwa kuzingatia aina ya wachezaji walionao Galatasary. 

Chelsea Description: Chelsea FC  20:45Galatasaray  (1:1)